Jamaa anajiita Future JnL, binafsi nimeanza kumsikia mwaka huu, na nimepitia ngoma zake Tatu tu na mwisho wa siku nimejikuta nikirudia rudia kusikiliza na kutazama video yake ya Without You, Jamaa anajua kucheza na sauti na swagger katika video basi imekua bonge la track. Lakini pia nimemcheki katika ngoma aliyoshirikishwa na mwanadada Rapper anajiita Y.T ngoma inaitwa Funzo
Nikaona si mbaya kushare nawe ngoma hizi mbili, zote akiwa ame release mwaka huu waa 2015
Hii inaitwa Kubali, (audio)
N hii pia inaitwa Crazy, sikia jamaa anavojua kucheza na sauti humu
Cheki na hii Video pia, Without You, Video imefanywa na Kwetu Studios