Thursday, October 1, 2015

Kama Bado Haujamsikia Jamaa Anajiita Future Jnl, Sikia Kipaji Hiki Pia (Audio & Video)


Jamaa anajiita Future JnL, binafsi nimeanza kumsikia mwaka huu, na nimepitia ngoma zake Tatu tu na mwisho wa siku nimejikuta nikirudia rudia kusikiliza na kutazama video yake ya Without You, Jamaa anajua kucheza na sauti na swagger katika video basi imekua bonge la track. Lakini pia nimemcheki katika ngoma aliyoshirikishwa na mwanadada Rapper anajiita Y.T ngoma inaitwa Funzo



Nikaona si mbaya kushare nawe ngoma hizi mbili, zote akiwa ame release mwaka huu waa 2015

Hii inaitwa Kubali, (audio)

N hii pia inaitwa Crazy, sikia jamaa anavojua kucheza na sauti humu




Cheki na hii Video pia, Without You, Video imefanywa na Kwetu Studios









Thursday, August 13, 2015

Wakati Wengi Wakilalamikia Mitandao Ya kijamii, Hii Ni Hatua Iliyochukua Serikali ya India Kwa Mtu Huyu Baada ya Kushare Picha Chafu Za Mtoto Mdogo

Hii imetokea katika mji wa Chennai, nchini India. Ni mji ulio na Viwanda vingi pia ni mji mkubwa wa kibiashara. Engineer mmoja katika mji huo alifikia hatua ya kushare picha chafu, tena zikimuhusisha mtoto mwenye umri mdogo, akitumia group ya Watsapp ambayo inatumiwa na wafanyakazi katika kampuni anapofanyia kazi pia. Jamaa amekua chini ya ulinzi wa polisi ni baada ya mwanamke mmoja ambaye pia yupo katika group hilo, kukerwa na kuamua kutoa taarifa katika vyombo husika, na serikali haikuchelewa kumtia rumande, akatoe maelezo zaidi huko.
Chombo maalumu kinacho husika na mambo ya kimitandao na kutetea mambo machafu wanyo kua wakifanyiwa watoto wadogo Protection Of Children From Sexual Offences (POSCO), Ndio waliohusika katika uchunguzi wa sakata zima, haikuishia hapo tu jamaa wakagundua kwamba simu ya Engineer huyu ndio iliyohusika katika kuchukua picha pamoja na videos, sababu zilizojitosheleza kabisa kmuweka jamaa chini ya ulinzi.

Pia serikali ya India haukushia hapo tu, imetoa agizo kwa Internet providers kuzima sites zote zinazo jihusisha na kupost picha za ngono za watoto wenye umri mdogo.

Hii imekua kero kubwa pia hapa bongo, wazazi wamekua wakilalamikia sana mitandao hii ya kijamii, kwani inawafanya watoto kuiga mambo mengi sana yanyo onekana katika mitandao, lakini limekua gumu sana katika utendaji, kwani bado watu wanapata picha na video za namna hii ambozo pia zipo katika viganja vya watu wengi. Na imekua rahisi sana kwa vijana na watoto wadogo kuvifikia na kutazama kadri wanavyo jisikia.

Monday, August 3, 2015

Sikia Alicho Fanya Ben Pol Katika hii "All Of Me/Drunk In Love Cover" (Audio)


Tumesikia ngoma kibao walizo fanya undergrounds kibao, haswa kwa wale wanao yafuta attention kupitia Youtube na social networks, Lakini pia mastaa kibao wamekua wakitumia ngoma hizi zilizo chukua nafasi katika mitandao na stations nyingi duniani.
Hii sasa ni ya Ben Pol, the king of RnB ambae story iliyopo town kwasasa ni ile ya kuitwa katika muendelezo wa zile seasons za Coke Studio kufanya yale kama walofanya kina Dimond, Jide, Joh Makini na wengine. Ni Music cover ya "All Of Me na Drunk in Love" unaweza kudance humu ndani.

Isikilize Hapa


Thursday, July 23, 2015

Aiseee Nuhu Na Shilole, Nia Yao Kumbe Ilikua Hii (Audio)


Siku kadhaa hapa nyuma tuliona majibizano flani @Instagram, wengi tukidhani kwamba jamaa wamezinguana tena, kumbe majibizano yote ilikua ni kama lyrics hivi, ya ngoma yao hii inayo itwa Ganda la Ndizi.
Imekua kawaida kusikia mambo kama haya kwa mastaa kadhaa, nadhan ni namna tu ya kupata attention kutoka kwa mashabiki, na mda mwingine ina tengeneza makundi kabisa, laikini kumbe nia ya wawili hawa ilikua tofauti kabisa. Kitu ambacho binafsi nadhani ni kizuri, unawapa watu kitu ambacho hata hawaku tarajia.

Ila sasa wakati mwingine inabidi watafute namna nyingine, kwani ni mara nyingi sasa wamekua kama na ogimvi hivi lakin kumbe ni michezo tu

Sikia Ganda la Ndizi hapa

Wednesday, July 22, 2015

Top Ten Ya Billboard 200, Album Ya Tyrese Yashika Namba Moja



Tyrese kasshika nafasi ya kwanza na Album yake ya "Black Rose" ambayo ipo sokoni tangu July 10. Hii inakua Album ya Sita ya Tyrese. Jamaa kampiga chini Meek Mill na album yake ya The Dreams Worth More Than Money iliyoshika namba moja kwa wiki mbili zilizopita. Wakati mwana dada Taylor Swift akishilia nafasi ya tatu na album yake ya 1989

Tyrese Amekua akifanya vizuri katika movies pia, we know how crazy he is akiwa kwa Camera, tumemuona katika Fast & Furious 7, movie ambayo inafanya vizuri sana sokoni. Hii ni ishara kwamba pocket ya Tyrese si mchezo kwa sasa.

Billboard 200 Top 10
1. Tyrese- Black Rose
2. Meek Mill- Dreams Worth More Than Money
3. Taylor swift- 1989
4. Kidz Bop Kids- Kids Bop 29
5. Ed Sheran- x
6. Sam Hunt- Montevallo
7. R5- Sometime Last Night
8. Meghan Trainor- Title
9. Maroon 5- V
10. Sam Smith- In The Lonely Hour

Ulilijua Hili, Diamond kutia Calenda Collabo Na D'Banj (Audio)




Issue nzima imezungumziwa leo katika XXL ya Clouds Fm, kumbe jamaa ilikua wafanye kazi kitambo na D'banj akawa anaona kama clue nzima ya Diamond pamoja na mameneja wake wanamrushia ivi.

Jamaa anasema labda ni kwasababu Diamond anakua akimake mkwanja mrefu kili iitwapo siku, na anasikia kila siu yupo Nigeria, kaomba apewe taarifa wafanye kazi watu waenjoy.

Msikia hapa D'banj pamoja na Majibu ya Diamond, pia kuna issue inaweza kuwapo inamuhusu Davido na Alikiba


Dakika Mbili Na Nusu Za "Faster" Ya Kid Ink (Video)


Faster ni ngoma ya pili katika Album ya Kid Ink "Full Speed", ambayo ipo sokoni tangu mwezi January. Ngoma yenyewe ina dakika mbili na sekunde ishirini na saba tu, katika hii Video jamaa ameshare nawe dakika mbili unusu. Katika Album hiyo kuna tracks kali kama Body Language, humo ndani kuna Usher, na nyingine kali kibao.

Na kuanzia August 25 jamaa atakua anaanza world tour "One Hell Of A Night Tour"

Nadhani jina la ngoma limeendana kabisa na mda ambao unaweza enjoy Video hii, lets go now, FASTER!!!!!!!!